Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amesema kuwa yeye ni miongoni mwa watu wanaopitia changamoto kubwa hususani kwenye mahusiano yake pale anapotoa support kwa wasanii wenzake.

Wolper amekiri kuwa kila akipost kukubali kazi za wasanii huwa inampa shida kwenye mahusiano yake kutokana na mtazamo uliopo kwa wasanii.

”Unajua inaniharibia sana mpaka natamani kuacha ila nimezoea inabidi tu niendelee na pia mashabiki wanavyotukana ukifanya jambo inaonekana kama kweli sasa kiasi kwamba mtu unayekuwa naye anakosa imani” – Wolper.

Miongoni mwa wasanii aliopost kazi zao na kupata mitazamo tofauti ni Marioo, Harmonize, Ibraah na wengine lakini analazimika kufanya hivyo kwasababu nyimbo zao unakuta zimemgusa yeye au zinakuwa na ujumbe wa kuelimisha zaidi.

Kwa upande mwingine Wolper amesema kwasasa filamu hazilipi kama ambavyo kazi yake ya ubunifu wa mavazi inavyompaka pesa lakini pia ameona soko kwenye series hivyo anaweza kufanya chochote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *