Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka na kusema kuwa wasanii wake waliotoka kwenye lebo yake walikuwa hawana mikataba ndiyo mana hakuwazuia kuondoka.
AliKiba amethibitisha Cheed na Killy kuondoka kwenye label ya Kings Music Records bila kusema sababu ya wasanii hao kuondoka ndani ya lebo hiyo.
Kiba amesema ni kweli wameondoka na kwa sasa label hiyo imebakiwa na wasanii Wanne tu kwasasa ila hana kinyongo na wasanii hao baada ya kujitoa kwenye lebo yake.
Kiba ameeleza kwamba wawili hao walimfata nyumbani kwake usiku wa saa 8 na kuzungumza ambapo mazungumzo yao ya kumuaga yaitumia dakika 5 tu.
Kisha ilipofika saa 10 alfajiri ya kuamkia jana (April 14) walianika ujumbe wa kujiondoa rasmi Kings nami bila tatizo nimewaruhusu kuondoka.
–
“Walinifuata jana usiku saa 8 kasoro, wakaniambia walichotaka, nikawaambia kila la kheri. Saa 10 wakapost kwamba wamejiondoa kwenye Label.” amesema Kiba.
Kiba ameeleza kuwa anawatakia mema waendapo kwani wameiva vyema kwa muda walioutumia hapo, pia Kiba amesema kuna pesa nyingi ambayo aliiwekeza kwao lakini ni kama ametoa sadaka tu.