Mwanamuziki wa Nigeria, Burna Boy alikuwa sehemu ya mastaa wa dunia ambao walipigiwa simu na rapper Diddy kujumuika pamoja LIVE kupitia Instagram akaunti yake.
Diddy amewapigia simu na kuongea nao kwa ajili ya kuchangisha fedha mahususi kwenda kwa wahudumu wa afya wakati wa mapambano dhidi ya Corona.
Burna Boy staa kutoka Afrika alizungumza mengi na Diddy ikiwemo kumpa taarifa za COVID-19 kwa Nigeria na Afrika kwa ujumla.
Wengine ni pamoja na Jennifer Lopez, Drake, LeBron James, Meghan Thee Stallion, DJ Khaled na wengine kibao ambao wamekubali kuchangia kiasi hicho.
Katika kampeni hiyo, Diddy kupitia ukurasa wake wa Twitter alitangaza kupokea michango kiasi cha zaidi ya ($3M) sawa na takribani Bilioni 6.8 za Kitanzania huku pia CEO wa Twitter, Jack akichangia kiasi ($2M) kusaidia wahudumu wa Afya.