Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amefunguka na kusema kuwa alikuwa hajui kama mpenzi wake Billnass angemvarisha pete ya uchumba kwa hivi karibuni.
Billnass alimvisha Nandy pete hiyo ndani ya kipindi kinachorushwa kupitia Televisheni ya TVE ambapo baadhi ya watu walidai kuwa inawezekana ni maigizo siyo halisi.
Nandy amesema kuwa, alikuwa hajui kama angevalishwa pete siku hiyo, ilikuwa ni ‘tukio la kushangaza’ kwake licha ya kwamba huko nyuma aliwahi kukiri kuwa ana mpenzi na wako mbioni kufunga ndoa ambaye ndiye huyo.
Nandy amesema kuwa “Hii ni pete ya ukweli siyo kiki kama wengi wanavyosema, sikujua kama nitavishwa pete, lakini kama mlinifuatilia zamani nilisema kuwa nina mtu na ni kwamba tuna matarajio ya kufunga ndoa na pia watu wameshajua ni nani, basi mimi nashukuru,”.
Kwa muda mrefu, Nandy na Billnass wamekuwa wakikanusha kuwa kwenye uhusiano baada ya kutengana mwanzoni na kila mmoja kuchukua hamsini zake, lakini sasa ni wachumba rasmi.