Albamu ya msanii wa Bongo Fleva, Harmonize ‘Afro East’ imerejea tena mtandaoni baada ya kutoweka kwa ishu zinazohusiana na haki miliki.
Afro East, iliyozinduliwa Machi 14, mwaka huu, ilifanikiwa kufanya vizuri katika mitandao ya kuuza, kusikiliza na kupakua muziki duniani lakini juzi ikatoweka ghafla jambo lililozua taharuki miongoni mwa mashabiki zake.
Harmonize alisema: “Niwaombe samahani mashabiki zangu wote kwa albamu yetu, Afro East kupotea kwenye ‘platform’ zote lakini Mungu ni mwema tayari imerudi kwenye mitandao ya Apple Music.
Pia Harmonize ameendelea kusema kuwa albam hiyo itaendelea kupatikana katika mitandao ya Spotify, Tidal, Audiomack, Boomplay Music na YouTube.”