Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amewataka vijana kukabiliana na changamoto wanazopitia katika maisha yao ili kufikia lengo la mafanikio.

”Kila kitu kinachotokea katika maisha yake kichukue kama changamoto , ni muhimu kukabiliana nacho na kuthibtishia watu kwamba unaweza kupambana nacho.

Wimbo wake ‘Never Give’ ama usikate tamaa unaelezea ujumbe wake kwa undani zaidi. Anasema kwamba kila kitu kilichopo katika kanda hiyo ni cha ukweli.

Kabla ya kuwa msanii maarufu nchini Tanzania , Harmonize alionekana kwa mara ya kwanza katika kipindi cha kuonyesha kipaji na aliambiwa na majaji kusahau kuhusu muziki.

Hatahivyo kwa bahati nzuri alipuuzilia mbali ushauri wa majaji hao wa muziki na kuendelea na kile alichoona ni kipaji.

”Nilijua kwamba nilikuwa na kipaji hivyobasi niliendelea kujifunza muziki licha ya ushauri wa majaji wale”.

Hatimaye kujiamini kwake kulizaa matunda na hii leo Harmonise anajivunia mamilioni ya wapenzi wa muziki wake katika mtandao wa You Tube.

Licha ya msanii huyo kuchukuliwa na nyota wa muziki wa bongo fleva na msanii Diamond Platinumz kwa sasa ameamua kufanya muziki wake binafsi baada ya kujiondoa katika lebo ya Wasafi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *