Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amewataka mashabiki zake wasimpande kichwani kwa kumuuliza kwanini hapati mtoto na mumewe kwa sababu hawajui ana matatizo gani.

Shilole amewataka mashabiki zake wawe wavumilivu na wasijaji maisha yake, bali wafuatilie kazi na biashara zake.

“Tutapata mtoto tu, halafu hayo sio mafungu ya nyanya kwamba yanawekwa tu pale, ni baraka kutoka kwa Mungu, bado siku haijafika hata mimi natamani sana kupata mtoto, naamini ataleta kheri kuhusu mashabiki zangu siwajali kwa sababu wao hawalali na mimi” amesema Shilole.

Pia Shilole ameendelea kusema “Wao wanajua kama nina matatizo gani au walishanipeleka hospitali wakajua kama nina shida gani.

Kwa upande mwingine mwanamuziki amewataka mashabiki zake wawe wavumilivu wasijaji maisha yangu, waangalie muziki wangu na biashara zangu mambo ya ndoa yangu na kutozaa hayawahusu nikipata waseme Inshaalah, nikikosa waseme Hewala”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *