Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amefunguka na kusema kuwa anatarajia kuwa mke hivi karibuni pia ameeleza sababu ya wasanii wengi wa kike wasiingine kwenye ndoa.

Katika akaunti yake ya Instagram mwanamuziki huyo ameandika kuwa anatarajia kuingia kwenye ndoa lakini hakusema lini wala hakumtaja mwanaume atakayefunga naye ndoa hiyo.

Nandy ameandika “Kila mwanamke anastahili ndoa, wakati wa Mungu ni wakati sahihi sijui nitaolewa na nani aidha msanii au la ila tuombeane uzima nitaingia huko mwaka huu au mwakani” amesema Nandy.

Pia Nandy amesema wanawake wengi wanapanga mipango yao ya baadae kutokana na ratiba na kazi ambazo wako nazo zinasababisha wasiingie kwenye ndoa.

Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa “Sidhani kama sisi ni wagumu kuingia kwenye ndoa ila watu hawaingii kwenye viatu vyetu.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa hamjui ambayo yapo kwetu kuanzia ratiba, kazi ambazo tunazo sio kama hatuingii ila sababu ni kupanga mipango ya baadae ila siwezi kuwaongelea wengine kwa mimi sio muda mrefu nitaingia kwenye ndoa” ameeleza Nandy.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *