Afrika ni bara linalokuwa kwa kazi kumuziki kutokana na kila mwaka kuibuka na wanamuziki wapya ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya muaziki barani humo.
Wafuatao ni nyota Watano wa kuawaangalia katika mwaka 2020 kutokana na ubora wa kazi zao jukwaani kwa hivi sasa.
Sheebah Karungi (Uganda)
Akiwa na mafanikio ya kimuziki katika nchi yake ya Uganda, muziki wa Sheebah sasa unavuka mipaka.
Akiwa na sauti mahiri, Sheebah ni msanii mwenye malengo.
Kuanzia kushirikiana na wasanii wengine wa Kiafrika hadi densi, mtindo wake wa fasheni, anatumia talanta yake kuupeleka muziki wa Uganda kote dunaini.
Ni mwanamke mwenye uwezo mkubwa. Kimaisha yupo tu kama mwanamke mwingine yeyote wa kawaida, na ndio maana anaweza kuwasiliana vema na mashabiki wake.
Lakini anapokua jukwaani, anabadilika na kuwa Superstar – mahiri na mwenye umbo la kuvutia.
Joeboy (Nigeria)
Joeboy alipata umaarufu kwa wimbo wake Baby, ambayo ilitazamwa na watu milioni 18 katika kipindi cha miezi tisa kwenye mtandao wa YouTube.
Akiwa na sauti inayotoka moyoni na kujielezea kwa ustadi katika mtindo wa kipekee wa nyimbo zake, mwimbaji huyu wa Nigeria huwasilisha mistari ya nyimbo zake kwa mitindo ya Afrobeats na pop.
Muziki wake anaoutoa mmoja mmoja pia umekuwa ukipokelewa vema na wafuasi wake. Mei uliopita, muimbaji huyu alitoa wimbo ulioitwa Love & Light.
Anapata umaarufu haraka – kwa misingi ya nyimbo hizi mbili tu, na anakaribishwa kote Afrika na tayari ameshafanya onyesho la muziki wake nchini Uingereza.
Brian Nadra (Kenya)
Tumekuwa tukimfuatilia Brian Nadra tangu mwaka 2017 alipotoa single yake Leo. Anaelezea muziki wake kama “Sauti ya kijana wa mjini kutoka katika enzi ya smartphone yenye misingi ya kitamaduni”.
Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Kenya mwenye sauti ya kuvutia amejijenga binafsi kama balozi wa muziki wa pop wa Afrika Mashariki – hadi sasa, Kenya ina wanamuziki wengi wa wa kiume waliofanikiwa kimataifa.
Brian ana mtindo wa kipekee – huimba, na kurap pia ameweza hata kuimba R&B, na kuingia katika aina nyingine za muziki, mkiemo reggae hip-hop.
Innoss’B (Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo)
Kwa kutumia muziki wa kitamaduni wa Wakongo, Innoss’B ameweza kuleta sauti ya kisasa yenye ujana katika muziki wake.
Mwaka huu, muimbaji huyu alipasua mawimbi kwa single yake ya Yo Pe – akishirikiana na nyota wa Tanzania Diamond Platnumz. Katika kipindi cha miezi mitatu, video zake za muziki zilikuwa tayari zina utazamaji wa watu milioni 14 kwenye mtandao wa You Tube.
Innoss’B ameweza kujumuisha sauti ya muziki maarufu wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wa rhumba na R&B na Afrobeats.
Sho Madjozi (Afrika Kusini)
Hakuna kitakachomsimamisha Sho Madjozi. Mapema mwaka huu , msanii huyu wa hip-hop wa Afrika Kusini, alishinda tuzo ya BET ya Msanii bora mpya.
Utashi wa kile anachokifanya ndiyo inayompa msukumo msanii huyu- Ukisikia nyimbo zake au kutazama tamasha lake la muziki, ni wazi kuwa anafurahia kile anachokifanya na hisia hiyo pekee ina mvuto!
Analeta utofauti flani katika muziki wa Afrika Kusini. Tofauti hii inapatikana katika ala zake lakini pia anarap – kwa lugha kadhaa- katika mtindo wa – gqom.
Wengi miongoni mwa wasanii wa Afrika Kusini hulenga soko la nyumbani lakini ameweza kuwashirikisha muziki wake watu wengine duniani.
Wimbo wake uliopewa jina la mchezaji wa mieleka wa Marekani John Cena unawasisimua wengi.