Wimbo wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ‘Uno’ unapatikana tena katika mtandao wa Youtube baada ya kufungiwa na producer wa Kenya kwa madai ya kuiba beat.
Magix Enga mtayarishaji wa muziki kutoka Kenya ambaye alihusika kuifungia video hiyo ameomba msamaha kwa msanii wa Bongo Fleva, Harmonize kutokana na kitendo hicho cha kuiondoa video hiyo mtandaoni.
Mtayarishaji huyo wa muziki ameliondoka video hiyo katika mtandano wa Youtube kwa madai kwamba ameiba biti ya wimbo uitwao DUNDAING uliofanywa na msanii King Kaka kutoka Kenya.
Magix aliwasilisha malalamiko yake kwenye mtandao wa YouTube juu ya Beat ya wimbo wa Harmonize, UNO kufanana na mdundo wa wimbo wa DUNDAING aliyouandaa yeye na kuimbwa na msanii King Kaka.
Baada ya kikao cha muda mrefu na mawakala wa YouTube Afrika Mashariki Ngoma Magix Enga ametangaza msamaha kwa Harmonize na kuirudisha YouTube video hiyo ya UNO.
Magix Enga ameandika Kupitia akaunti yake ya Instagram; “With #CLEMO @Ngomma ✌️Growth of East African music is bigger than all of us. And for this reason i have decided that I will release my copyright strike on Uno by Harmonize. I have decided to forgive the guy🇹🇿 Nitarudisha Uno by Harmoize Pale YouTube Wakati wowote.”
Baadaye akaandika tena; “Everybody say Uno ✌🏾🇰🇪🇹🇿 Now available on YouTube both audio and video.“