Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amesema kuwa wosia alioachiwa na Ruge ni kutumia akili, kuwa na mipango ya maisha na kuelekeza nguvu katika muziki wake.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Ruge Mutahaba iliyofanyika kijijini kwao Bukoba siku ya jana.
Ndugu jamaa na marafiki walijitokeza kwenye sherehe hiyo ya kumuenzi Ruge kutokana na mchango wake mkubwa katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva.
Kwa upande wake, mtoto wa marehemu Ruge, Mwachi Mutahaba, amesema; “Nandy alikuwa na urafiki na baba yangu na nimeanza kumjua kupitia hivyo, na pia kwa baba alikuwa ni msanii wa THT na alikuwa ni mpambanaji kwenye industry ya muziki wa kizazi kipya, kwa hiyo ilikuwa namheshimu.
Pia “Kwa familia tumemfahamu Nandy kama rafiki wa baba yangu na ni mtu aliyekuwa anamheshimu sana baba, sisi tumeamua kumheshimu na yeye kwa jinsi anavyotuheshimu sisi na baba yangu,”.