Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesitisha malipo ya posho za kujikimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini ambao wanaofanya mafunzo kwa vitendo baada ya kubaini kuwepo na wanafunzi hewa zaidi ya 1000 vyuoni.
Prof. Ndalichako amesema wizara yake imezuia posho hizo kwa muda wa wiki mbili wakati wizara hiyo ikiwa inafanya uhakiki ili kuwabaini wanafunzi hewa zaidi pamoja na wahusika kuwachukulia hatua za kisheria.
Pia Prof. Ndalichako amewaagiza wakuu wote wa vyuo kuwasilisha taarifa za wanafunzi wao wizarani ili zoezi la kukagua na kubaini uahalali wa wanafunzi hao kuwepo vyuoni na wale watakaoonekana kuwa wana sifa watapatiwa posho zao za kujikimu mapema na kuendelea na masomo yao chuoni.