Muigizaji wa Bongo Movie, Esther Kiama amesema kuwa mapedeshee wa mjini hivi sasa hawana dili kama zamani kwani wasanii wengi wa kike hawaangalii pesa bali wanataka mapenzi ya kweli.
Kauli ya muigizaji huyo imekuja baada ya kudaiwa kuwa siku hizi wasanii hawana mapedeshee kama zamani na ndiyo mana hawana hela kama walivyokuwa zamani.
Ester amesema kuwa mastaa wengi wamegundua mapenzi ya kweli hayapo kwa mapedeshee ambao walikuwa wanawatumia tu kupitia hela zao.
Muigizaji huyo amesema kuwa zamani mapedeshee walikuwa wakitumia mifuko yao kuwarubuni mastaa mbalimbali lakini sasa mambo yamebadilika tofauti na hapo awali walikuwa wanawarubuni kwa pesa zao.
Pia amesema kuwa wasichana wasasa hawatazami pesa bali mapenzi ya kweli na ndio maana ukichunguza utaona mastaa wanatoka na wanaume wa kawaida sana.
Wasanii wengi wa kike wamekuwa wakitajwa kuwa na mahusiano na wanaume wenye pesa wanaojulikana kama mapedeshee.