Aliyekuwa meneja wa Yamoto Band Mkubwa Fella amefunguka na kusema kuwa ameshtushwa na taarifa za kuacha kwa Aslay na mpenzi wake Tessy.
Fella amesema kuwa ameshangazwa na taarifa hizo kuwa moja ya wasanii walikokuwa wakiunda kundi hilo amb ae ni aslay ameachana na aliyekuwa mpenzi wake a siku nyingi ambae pia ni mama wa mtoto wake mmoja.
Mkubwa Fella anasema kuwa taarifa hizo alikuwa haziamini hata kidogo na kwamba hakuona kama kuna umuhimu wa kuzifatilia kwa sababu zilikuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii tu.
Mkubwa Fella amesema atakuwa tayari kufanya usuluhisho endapo wawili hao wataamua kutaka kumjulisha tatizo hilo na sio kubeba habari kutoka katika mitandao ya kijamii kwa sabab habari hizo mara nyingine huwa sio za kweli.