Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol ameamua kuthibitisha mahusinao yao baada ya kuamua kwenda ukweni kwa ajili ya kufanya utambulisho na mpeniz wake anaejulikana kama anerlisa.

Msanii huyo ambae aliingia katika mahusiano ya kimapezi na mwanamke huyo siku si nyingi zilizopita wameamua kuhararisha mahusiano hayo na kuamua kujitambulisha kwa wazazi hatua ambayo inaleta msukumo wa ndoa.

Ben pol atakuwa mwanamuziki wa kiume anaeongeza idadi ya wasanii wanaokwenda kuoa nje ya nchi na kuacha wasichana wa kitanzania.

Mwanamuziki huyo ameshukuru kupelekwa ukweni kwao na kujitambulisha kwa ndugu wa mpenzi wake nyumbani kwao nchini Kenya.

Uhusiano wa wawili hao umeanza toka mwaka jana ambapo walionekana pamoja nchini Dubai na sehemu mbali mbali wakiwa pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *