Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameweka wazi dili lake jipya alilosaini na kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi Tanzania.
Diamond alisaini mkataba wa kwanza na kampuni hiyo kupitia kinywaji cha Mirinda ambapo walikuwa wadhamini wakubwa wa tamasha la Wasafi Festival.
Diamond amezungumza na waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa Serena Hotel uliopo Posta jijini Dar, wakati wa utambulisho wa kinywaji kipya cha Mkubwa Wao ambacho kilizinduliwa tangu Januari 21.
Msanii huyo ameoneka kuwa na bahati ya kupata ubalozi kupitia makampuni mbali mbali hapa nchini kutokana na kufanya vizuri kwenye muziki wake.