Mwanamuziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz amefunguka na kumwagia sifa kibao Mpenzi wake ambaye ni mrembo kutoka Mombasa Kenya Tanasha Donna Oketh.
Diamond amemwagia sifa mke wake huyo mtarajiwa na kusema mbali na mambo mengine Lakini mrembo huyo anajua sana kupika.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa mwanamke huyo ndiyo pekee aliyemuonesha yupo makini na ana sifa zote za kuingia naye kwenye ndoa.
Pia Diamond ameweka wazi nia yake ya kufunga ndoa na mwanamke huyo kutoka nchini Kenya ambaye anaonekana kuziba vizuri pengo la Zari the boss lady.
Vile vile amesema kuwa Tanasha ana sifa zote ambazo mwanaume yeyote aliyekamilika angetamani awe mkewe.
Diamond alitangaza kufunga ndoa na Tanasha muda mfupi tu Baada ya Kukutana ambapo mara ya kwanza ndoa ilitakiwa ifungwe mwezi wa pili katika siku ya wapendanao Lakini imesogezwa mbele.