Mwanamuziki wa Marekani, Chris Brown anakabiliwa na tuhuma za kumbaka mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 24 huko Ufaransa usiku wa Januari 15 mwaka huu.

Mwanamke huyo amesema kwamba alifanyiwa tukio hilo baada ya kukutana na msanii huyo club huko ufaransa, na akamkaribisha chumbani kwenye hoteli aliyofikia iliyokuwa inajulikana kwa jina la ‘Mandarin Oriental Hotel.

Mwanamke huyo amefunguka kwamba chumba walichotumia na Chris Brown ndipo alipomfanyia kitendo hicho  humo.

Chris Brown (Breezy) hajasema neno lolote juu ya taarifa hizo.

Taarifa zilizotolewa na chanzo cha Ufaransa cha  ‘Closer’ kinaeleza kwamba Breezy yupo chini ya upelelezi wa polisi kuhusiana na tuhuma hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *