Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amefunguka na kusema kuwa mwakani ana ndoto ya kuzaa mtoto baada ya kuolewa.

Lulu Diva amefunguka kuwa kwa kazi yake ya muziki anayoifanya hivi sasa,  kufanya kitu ambacho huko mbeleni hakitampa kikwazo kama kupata mtoto mapema ili akiwa anaendelea kumtafutia maisha, yeye anaendelea kukua.

Mwanamuziki huyo amefunguka na kusema kuwa ni vizuri sana kujipangia malengo ya kimaisha na ndiyo mana amepanga mwakani lazima azae kwani wakati umeshafika.

Pia Lulu Diva amesema kuwa anachokitaka mwakani kwa sababu maisha yenyewe ni mafupi hivyo ana budi kupata mtoto.

Mwaka huu ulianza kwa tetesi za Lulu Diva kuolewa lakini taarifa hizo ziliyeyuka Baada ya Lulu Diva kuachwa na mchumba Wake Baada ya kuenea kwa tetesi za mahusiano na Rich Mavoko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *