Swahili Fashion Week ni maonyesho ya mtindo yanalofanyika kila mwaka nchini Tanzania kwa ajili ya kukuza mitindo hapa nchini.
Tamasha hili lilianzishwa Tanzania na mbunifu wa mavazi nchini Mustafa Hassanali mwaka 2008 na mpaka sasa hivi limefikisha mwaka wa 10.
Maonyesho haya ya mitindo inatoa fursa kwa wabunifu wa mtindo na vifaa kutoka kwa nchi zinazozungumza lugha ya kiswahili na zaidi pia inaonesha vipaji vyao.
Swahili Fashion Week inalenga kusisitiza kwamba mtindo ni sekta ya ubunifu inayozalisha kipato wakati huo huo kukuza dhana inayofanywa Afrika.
Tamasha hili la mitindo nchini limefanyika kwa siku siku tatu kuanzia November 30 hadi December 2 mwaka huu katika viwanja vya makumbusho ya taifa Posta jijini Dar es Salaam.