Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Amber Lulu amefunguka sababu za kurudisha penzi kwa mwanamuziki wa nchini Kenya, Prezzo baada ya kumwagana naye miezi kadhaa iliyopita.
Amber Lulu aliweka wazi kuwa huko nyuma aliteswa kuumizwa na mara nyingine kuchezea vitasa kutokana na mapenzi, lakini alipoingia kwa Prezzo alijiona yuko peponi hivyo walipoachana, aliona kuna sababu ya kurudisha mapenzi kwake.
Mwanamuziki huyo alipata maumivu sana kwenye mapenzi alipoachana na mpenzi wake huyo na alidhalilishwa na kuumizwa.
Amber Lulu amesema kuwa alipigwa sana, yaani alikuwa kama teja lakini siyo wa kuvuta unga, bali ni wa mapenzi, lakini kwa Prezzo alikuta tofauti.
Pia amefunguka na kusema kuwa ameona arudishe penzi kwa nguvu zote kwa mwanamuziki huyo kutoka nchini Kenya.