Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja amefunguka na kuweka wazi kuwa kwasasa amekata tamaa ya kuzaa mtoto mwingine kutokana na umri wake kuwa mkubwa.
Kajala amesema kuwa, kipindi cha nyuma alikuwa akisaka mtoto mno, lakini ilishindikana hivyo umri unasogea na pia mtoto wake ameshakua ni msichana mkubwa hivyo inabidi aangalie maisha mengine na siyo kuzaa tena.
Kajala ameweka wazi kuwa kwa sasa ana umri wa miaka 36 hivyo anajiona tayari ameshakuwa mtu mzima sana hivyo hawezi tena kuzaa kilichobaki ni kumlea mtoto wake.
Kajala amezaa mtoto mmoja na mtayarishaji mkongwe wa muziki wa Bongo fleva P Funk Majani, mtoto huyo anajulikana kwa jina la Paula.