Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego kesho atakutana na uongozi wa Baraza la Sanaa nchini BASATA kujadili mwenendo wa kazi zake za Sanaa.

Nay amesema kuwa ni kweli BASATA wamemuita siku ya kesho kwa ajili ya kujadili kazi zake za Sanaa anazofanya siku za hivi karibuni.

Mwanamuziki huyo amedai kuwa alipewa barua na Baraza hilo ambayo ndani yake lilimtaka afike ofisi za BASATA kesho siku ya Jumanne.

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limempatia Nay wa Mitego barua yenye ukarasa mmoja iliyokuwa ikielezea ajenda ya kukutana naye kuwa ni kujadili mwenendo ya kazi zake.

Nay wa Mitego alikaa kimya kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kufungiwa kazi yake na BASATA na kuamua kurudi kwa kuachia Ngoma ya Alisema ambayo nayo imeonekana kuleta utata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *