Mwanamuziki wa Bongo Movie, Vicent Kigosi maarufu kama Ray ameibuka na kukiri kuwa anatamani sana mtoto wake Jaden aende akapate elimu katika nchi za nje.
Ray amefunguka kuwa yupo katika mapambano makubwa ya kufa na kupona ili kuhakikisha mtoto wake wa kipekee Jaden anaenda kupata elimu bora kabisa.
Ray alisema si kwamba Tanzania hakuna shule bora kwa hapa nyumbani lakini ndoto zake anatamani mwanawe asome nje ya Tanzania kama ambavyo amejiwekea toka awali.
Jadern ni mtoto wa kwanza wa Ray aliyezaa na Msanii mwenzake wa Bongo movie mwanadada Chuchu Hansy.