Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Hamisi Mwinjuma maarufu kwa jina la Mwana FA ameteuliwa na Serikali kuwa mjumbe wa Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Uteuzi huo ambao umeanza tangu Oktoba 5, 2018, umetangazwa leo ikiwa ni siku 17 zimepita tangu Rais Dkt. John Magufuli alipomteua Bw. Habbi Gunze kuwa Mwenyekiti wa baraza hilo.
Waziri wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ana dhamana ya kuteua wajumbe wa Bodi baada ya Rais kumteua Mwenyekiti wake.
Wasanii walioteuliwa miongoni mwa wajumbe hao ni msanii wa hip hop, Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA pamoja na muigizaji Single Mtambalike maarufu kama Richie.
Wajumbe hao wataitumikia bodi hiyo kwa muda wa miaka mitatu. Maelezo zaidi ya uteuzi huo yapo kwenye taarifa hapo chini.