Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amesema serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuwafutia umasikini watanzania ikiwa ni pamoja kwa kuwafikishia umeme katika maeneo yote ya vijijini.

Muohongo: Akizungumza na baadhi ya viongozi kwenye mktano uliofanyika Tanga.
Muohongo: Akizungumza na baadhi ya viongozi kwenye mkutano uliofanyika Tanga.

Waziri Muhongo amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kuendeleza usambazaji wa umeme vijijini uliofanyika katika kijiji cha Kudizinga, wilayani Handeni mkoani Tanga.

Waziri huyo amesema serikali haiwezi kufuta umasikini wa watanzania endapo hawatakuwa na umeme hivyo wamedhamiria kufikisha umeme wa uhakika katika maeneo yote ya vijijini ili kufuta umasikini unaowakabili wananchi wengi waishio maeneo hayo.

Pia Mkuu wa Mkoa wa Tanga amewataka wananchi wa mkoa huo kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo badala ya kujiingiza katika mambo ya kisiasa na kuwachelewesha katika juhudi za kujiletea maendeleo nchini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *