Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linah Sanga anadaiwa kuachana na mpenzi wake aliyezaa naye mtoto mmoja anayejulikana kama Mchomvu baada ya wawili kutoonekana wakiwa pamoja kwa muda mrefu.
Penzi la wawili hao limevunjika wakati wakiwa kwenye taratibu za kufunga ndoa hivyo kushindwa kutumiza lengo lao la ndoa hiyo.
Linah na mzazi mwenzake walianza kuingia kwenye mgogoro baada ya mwanadada huyo kujifungua mtoto wake wa kwanza mwaka jana.
Ilisemekana kwamba, mara kadhaa wamekuwa wakikalishwa chini na kuyamaliza mambo yao kichinichini bila mtu yeyote kujua kisha wanaendelea na uhusiano kama kawaida.
Inadaiwa kuwa ugomvi wa wawili hao mara nyingi ulikuwa ni wivu wa kimapenzi hivyo hicho ndicho kilichosababisha uchumba wao huo kuvunjika ambapo mpaka sasa kila mmoja anamuona mwenzake mchungu.