Mwanamitindo maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe amemtaka Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta kuhalalisha bangi.

Huddah ameomba mtu aliyekaribu na Kenyatta kumfikishia ujumbe huo kuwa kabla ya kura ya maoni Rais Kenyatta ahalalishe matumizi ya kilevi hiko kinachotumiwa na vijana wengi nchini humo.

2017 hoja hiyo iliungwa mkono na Wakenya zaidi ya 1,400 mara baada ya mtafiti Gwada Ogot kuwasilisha ombi lake mbele ya Bunge la Senet na kubainisha kwamba matumizi ya bangi kiafya yana faida nyingi ikiwemo kusaidia kuimarisha hali ya uchumi nchini.

Aidha, sheria nchini Kenya inapiga marufuku utumiaji wowote wa bangi na kwamba mtu yeyote atakayepatikana akitumia dawa hiyo atashtakiwa kwa uhalifu.

Mtafiti Gwadahuyo alikiri kuvuta bangi wakati alipokuwa kijana,  amesema kuwa mataifa mengi katika bara Ulaya na Asia  na majimbo kadhaa nchini Marekani yamehalalisha utumiaji wa marijuana.

Ameorodhesha pia nchi za Colombia, Mexico, Jamhuri ya Czech, Costa Rica, Ireland, Australia, Jamaica na Ujerumani miongoni mwa nchi zilizohalalisha matumizi ya bangi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *