Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja ameweka wazi kuwa ametumia zaidi ya Milioni kumi na Sita kununua vito vya thamani ikiwemo saa ya mkononi.
Kajala ameteketeza Milioni kumi na Sita kununua saa yake ya mkononi ambayo inamchanganyiko wa dhahabu na almasi pamoja na bangili ambazo amedai alizipenda sana.
Kajala alisema kuwa, alinunua saa hiyo na bangili wakati akiwa nchini Dubai na alifanya hivyo kwa sababu aliipenda sana seti hiyo na ni moja ya vitu ambavyo anapenda kuwa navyo.
‘Nikweli nimenunua saa hiyo nchini Dubai, kwani nimeipenda sana hivyo nikaamua kununua bila kujali gharama yake’ Alisema Kajala.
Kajala anatajwa kuwa na mkwanja mrefu kutokana na kazi yake ya ubalozi wa Biko Lakini pia kupitia sanaa ya uigizaji iliyomtambulisha vizuri hapa Bongo.