Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Malaika amefunguka na kusema kuwa hawezi kumuanika mpenzi wake hadharani ingawa anapata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume wengine.

Malaika ambaye alijizolea umaarufu baada ya kusikika kwenye ngoma ya Chege ‘Uswszi Take away’ amefunguka kuwa hawezi kumuweka wazi mpenzi wake.

Lakini pia Malaika amefunguka kuwa anapata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume hasa kwa sababu wa urembo wake.

Malaika ameongelea pia ukimya wake Kwenye tasnia ya Bongo fleva ambapo amesema alikaa kimya kwa muda kutokana na majukumu yake nje ya muziki.

Kwasasa mwanamuziki huyo amesema kuwa anatarajia kuja na kazi nyingine itakayomurudisha hewani baada ya kupotea kwa muda kwenye game la muziki wa Bongo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *