Staa wa muziki wa Singeli Dulla Makabila amefunguka na kudai anawashangaa wasanii ambao wameweka trend ya kwenda kuoa nje ya nchi huku akisisitiza kuwa hadhani kama ni ujanja.
Siku za hivi karibuni imetokea karibia wasanii kadhaa wa Bongo Fleva wameonekana wakienda kufunga ndoa nje ya nchi.
Wasanii kama Ali kiba aliyeoa binti kutoka Mombasa Kenya lakini pia Stamina aliyeoa mwanamke kutoka Rwanda Lakini pia Ay alimuoa Remmy kutoka Rwanda.
Lakini Dulla amewafungukia Dizzim Online kuwa haoni kama kuoa nje ya nchi ndio ustaa au ndio trend kwani anaamini mapenzi mapenzi tu utakapodondok ndio hapo hapo.
Lakini pia Dulla alifunguka ma kuweka wazi kuwa tangu ameachana na aliyekuwa mpenzi wake Husna Sajenti amekuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na wanawake kadhaa (zaidi ya mmoja) na kaweka wazi kuwa hana Mpango wa kuoa.