Magoli kutoka kwa Eden Hazard na Diego Costa yametosha kuipa ushindi Chelsea baada ya kuifunga West Ham United 2-1 kwenye mechi ya kwanza ya ligi kuu nchini Uingereza iliyofanyika katika uwanja wa Stamford Bridge.

Eden Hazard alikuwa wa kwanza kuiandikia Chelsea goli la kuongoza katika dakika ya 47 ya mchezo kwa njia ya mkwaju wa penati huku goli la West Ham likifungwa na James Collins katika dakika 77.

Chelsea walipata goli lao la pili kupitia mshambuliaji wake Diego Costa katika dakika 89 ya mchezo huo na kuipatia timu yake alama tatu muhimu kwenye mechi ya kwanza ya ligi kuu nchini Uingereza.

Chelsea: Baadhi ya wachezaji wakishangilia goli kwenye mechi dhidi ya West Ham.
Chelsea: Baadhi ya wachezaji wakishangilia goli kwenye mechi dhidi ya West Ham.

Chelsea walionekana kutawala sana mchezo huo mpaka kupelekea kushinda mechi hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Stamford Bridge.

Huo ni ushindi wa kwanza wa kocha mpya wa Chelsea, Antonio Conte kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza toka awe meneja wa timu hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *