Uongozi wa mwanamuziki wa Nigeria, Falz umesema haupo tayari kuiondoa video ya wimbo wa ‘This is Nigeria’ kwenye mtandao wa Youtube kama ilivyotakiwa na kikundi cha kiislamu cha ‘MURICO’.

Hayo yamejiri baada ya kikundi cha waislamu cha The Muslim Rights Concern (MURICO) cha nchini Nigeria kutaka wimbo wa mpya wa ‘This is Nigeria’ kutolewa Youtube kutokana na mahudhui ya kuwadhalilisha waislamu.

Uongozi huo umesema kuwa hakuna sehemu yoyote katika sheria za Nigeria inayokataza mtu kucheza akiwa amevaa Hijab hivyo kikundi hicho labda kina lengo lingine juu ya msanii wao.

Mmoja wa viongozi wa msanii huyo amesema kuwa hakuna sehemu sehemu yoyote nchini Nigeria inakataza kuvaa Hijab hivyo hawawezi kuitoa video hiyo kama wapo tayari waende mahakamani ndiyo itakuwa vizuri Zaidi.

Kikundi hicho cha kiislam kilimpa siku 7 rapa Falz kufuta video ya wimbo huo kwenye mtandao wa YouTube wakidai kuwa ameidhalilisha dini ya Kiislamu kwa kuwavalisha wanawake hijab na kuwachezesha kwenye video hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *