Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ferooz amesema kuwa kuna wakati anatamani kuacha muziki kama Q Chief lakini anashindwa kutokana muziki kuingia kwenye damu.

Uamuzi wa mwanamuziki huyo unakuja kufuatia kushuka kimuziki pamoja na kutopata sapoti kutoka kwa baadhi ya media mbali mbali.

Ferouz amesema kuwa sababu ya kutaka kufikia uamuzi huo ni kuonekana si kitu wakati ameutoa mbali muziki huo hadi kufikia uliopo.

Pia amesema kuwa licha ya kufanya muziki kwa takribani miaka 20 sasa amekuwa pia akifanya mambo mengine lakini mwisho wa siku anajikuta amesharudi kwenye muziki.

Wimbo wa mwisho kutoa mwanamuziki huyo unakwenda kwa jina la Najaribu ambao haujavuma sana kama alivyotarajia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *