Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Beka Flavour amefunguka kuwa anatamani sana hata kumfungia mbwa mpenzi wake Sophia.

 Beka amesema kuwa, amekuwa na mapenzi makubwa sana kwa mpenzi wake huyo kiasi ambacho anatamani kumuwekea ulinzi wa mbwa kila mitaa anayokatiza.

Beka amesema kuwa Mapenzi niliyonayo kwa Sophia wangu ni makubwa mno, natamani sana ningeweza kumlinda popote anapoenda awe na mbwa ili asisogelewe na mtu yeyote yule kwa sababu nampenda sana jamani.

Beka ambaye hata hivyo hana mpango wa kumuoa msichana huyo kwa sasa japokuwa anampenda hadi atakapoweka mambo yake sawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *