Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutoka WCB, Rayvanny ametangaza kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Fayma ambaye amezaa na mtoto mmoja.
Rayvanny anaweza kuwa msani wa kwanza kutoka katika lebel hiyo Kutangaza kufunga ndoa na kama ndoa hiyo itakamilika.
Pia atakuwa msanii wa kwanza kufunga ndoa na kukaa katika mahusiano yaliyodumu na yasiyokuwa na drama katika lebel hiyo.
Siku za nyuma kidogo msanii huyo aliwahi kuweka oicha nyingi zikimuonyesha akiwa amekwenda nyumbani kwao Mbeya ambapo alikwenda kumtambulisha mpenzi wake huyo na mtoto wao wa kiume.