Mwanamuziki nyota kutokea nchini Marekani, Nicki Minaj amebadilisha ratiba ya kuachia albamu yake mpya ambapo ilitakiwa kutoka Juni 15 mwaka huu.

 

Mapema mwezi huu katika onyesho la mitindo na mavazi Met Gala lililofanyika mjini New York, malkia huyo wa Hip Hop alisema albamu yake itatoka Juni 15 na itaitwa jina la Queen.

Kupiia mtandao wake wa Twitter, Nicki ameonekana kubadili muda wa kuachia albamu hiyo na kupanga kuiachia Oktoba 8, 2018.

Albamu ya mwisho ya Nicki Minaj ilikuwa inaitwa The Pinkprint (2014) ambayo ilifanikiwa kutinga namba moja kwenye chati za Billboard 200.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *