Muigizaji wa Bongo Movie, Steve Nyerere, amefunguka juu ya tuhuma za kusaliti ndoa yake na kuzaa na muigizaji Wellu Sengo. Kitendo ambacho kimesababisha mke wake kuondoka nyumbani.
Steve Nyerere amesema kwamba yeye ni mwanaume rijali na kuzaa nje ya ndoa sio kitu cha ajabu, na mke wake wala hajaondoka kama watu wanavyodai kwenye mitandao ya kijamii.
“Mke wangu yuko nyumbani, kakaa tuli katulia mtoto watu hana presha, kuna watu wangapi wamezaa nje!? Sasa mimi kwani sio mwanaume, kuna mwanaume mwenye kasoro duniani!? Labda shoga, mi ni mwanaume tena rijali, mwanaume ni yule anayeyimiza majukumu yake”,.
Kutokana na hilo Steve Nyerere ametaka watu kuacha kujadili mambo yasiyo ya msingi kwenye mitandao ya kijamii na kueneza habari za uongo, na badala yake wafanye kazi kujiingizia kipato.