Muigizaji wa Bongo Movie, Ester Kiama amefunguka na kusema kuwa tangu akumbane na mkasa wa kuleweshwa madawa ya kulevya amekuwa muoga na hamuamini mtu yeyote.
Ester aliweka wazi kwamba, maruweruwe ya madawa hayajamuisha vizuri ingawa alishakwenda hospitalini na kupewa matatibu, lakini amekuwa na wasiwasi hata wa kununua chochote dukani kinachohusiana na majimaji.
Amesema “Huwezi kuamini kabisa, hata kutoka nyumbani kwangu ninaogopa sana, nimekuwa muoga kupitiliza na sijui hii hali itaishaje kwa haraka, naona nimepata ugonjwa mwingine wa ajabu sana wa kuwa na wasiwasi,”.
Ester amekuwa katika hali hiyo baada ya juzikati kunyweshwa kinywaji chenye madawa ya kulevya na kuibiwa kila kitu alichokuwa nacho ikiwemo simu mbili na pesa.
Muigizaji amesema kuwa kwa upande wake hawezi kumuamini mtu yoyote katika maisha yake kwasababu watu waliomfanyia vitu hivyo ni watu wake wa karibu.