Mama mzazi wa msanii Diamond Platinumz hivi karibuni amekuwa katika headline karibia kila kona kutokana na skendo iliyokuwa ikisambaa katika mitandao kuhusu yeye kumpa kipigo mwanamke  anaesemakana kutoka kimapenzi na mwanae pekee ya kiume Diamond .

Inasemekana kuwa mama Huyo aliamua kumpa kichapo hamisa kutokana na kuwa hapendi Hamisa kuwa karibu na mtoto wake huku akisema kuwa hamisa hana adabu hivyo hafai kabisa kuwa mkwe wake.

Mitandao ya kijamii imekuwa ikiripoti na kumtafuta sana kuzungumzia swala hilo, lakini pia katika mitandao ya kijamii watu wengi wamekuwa wakimtukana mama huyo kwa kuwa amekuwa akijihusisha sana na maswala ya  mitandao na hasa kumfatilia sana mtoto wake ambae ndio amekuwa source ya matatizo yote.

Akiwa kama mama na mtu mzima watu wamekuwa wakimtaka mama huyo kauchana na mitandao lakini pia aache kufatilia maisha ya mtoto wake wa kiume.

Sasa mama huyo ameamua kuwajibu wanaomtukana katika mitandao na kusema kuwa hata yeye hapendi kufatiliwa na watu kwa sababu hayo ni maisha yake na familia yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *