Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford ameonyesha kukerwa na tabia za baadhi ya watu ambao wanatoa misaada na baadae kuwafanya wenzao kama matangazo.
Kuali hiyo ya muigizaji huyo inakuja kufuatia baada ya baadhi ya kutoa misaada kwa watu wasiojiweza lakini mwisho wa siku wanatangaza kama wamewasaidia.
Shamsa ameonekana kutupia jiwe hilo gizani ambalo tayari limempata ambaye alimkusudia. Shamsa amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instagarm.
Ameanza kwa kuandika “Kila mtu anapenda kusaidiwa lakini kuna misaada mingine mpaka mtu unajuta kwann umesaidiwa. utafanywa tangazo kila sehemu,utasemwa na kusimangwa kila sehemu,utafanywa mtumwa,hata kama akikuudhi itabidi tu umchekee”.
Pia ameongeza kwa kuandika “Huyo mtoa msaada atajiona Mungu MTU kwamba bila YEYE maisha hayaendi, hapo bado hajakubania sehemu utasema yeye ndo mtoa RIZIKI.
Ameongeza kwa kuandika “Misaada ya aina hiyo ni bora ikupite ufe na shida zako tu maana itafika sehemu utamsujudu yeye na kumsahau Mwenyezi Mungu”.