Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Godzilla amefunguka na kusema kuwa mahusiano yake ya kimapenzi siku zote yamekuwa ya siri na wala sio kila kitu kinapaswa kuongelewa katika mitandao ya kijamii.
Godzillah anazungumzia wimbo wake mpya ambao unaitwa stay wimbo ambao baadhi ya watu wamekuwa wakihisi labda anazungumzia mahusiano yake ya kimapenzi.
Pia Godzillah amesema kuwa wimbo huo ni maisha ya watu wanayaishi lakini sio kweli kwamba hayo ni mahusiano yake kwa sababu upande wake mahusiano yake yako sawa wala hana kinachomsumbua na kwasema kuwa wasije wakashangaa hata yeye akafunga ndoa kama ilivyotokea kwa Alikiba.
Godzila amesema kuwa ndoa ya Alikiba imkuwa inspirationkubwa sana kwa wasanii wengi waliopo katika mahusiano na hata wale wasiopo katika mahusiano kutokana na mahusiano hayo kuwa na usiri mpaka sio ya ndoa.
Godzilla amesema kuwa kama ikitokea anataka kuoa kila mmoja atafahamu ila hawezi kutangaza kwenye mitandao ya kijamii.