Muigizaji wa Bongo Movie, Wastara Juma amesema kuwa anawashangaa baadhi ya watu wanaomtukana mitandaoni kuhusiana na afya.

Wastara amesema kuwa watu hao umtukana kwa sababu picha anazoposti ni za siku nyingi (TBT) alipokuwa India na hakuna wa kumzuia kuposti anachokitaka.

Muigizaji huyo amesema kuwa, hakuna anayempangia cha kuposti na kinachomuumiza ni pale ambapo kuna watu wanachungulia akaunti yake kwa ajili ya kusubiri ataposti nini ili wamtukane.

Amesema kuwa “Sikuomba kuchangiwa ili nitukanwe, ilitokea tu kwa sababu ya matatizo. Kwa kifupi, wanaonitukana kwa sababu ya afya yangu, ninamuachia Mungu, kofi la Mungu ni kali sana maana sikuomba kuumwa ili nichangiwe na baadaye nitukanwe, ni mipango ya Mungu tu na atawaadhibu wanaofanya hivyo,”.

Hayo yote yameibuka baada ya Wastara alitupia picha inayomuonesha amewekewa mirija kichwani akiwa nchini India ambapo picha hiyo ilishambuliwa kwa matusi huku wengine wakidai kuwa safari hii hawachangii bila kujua kuwa ni picha ya zamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *