Muigizaji wa Bongo Movie, Esha Buheti amemtaka mwanamitindo maarufu Jokate Mwegelo, kuacha kumchukia kisa AliKiba kuoa nchini Kenya.
Buheti amesema kuwa ames-ikia kutoka kwa watu wake wa karibu kwamba mwanamitindo huyo anamchukia kwa sasa kutokana na kuwa karibu na Kiba kwenye harusi yake na mrembo Amina Khaleef wa Kenya.
Amesema kuwa “Mimi ni kama bendera tu nafuata upepo kwa hiyo wa kumchukia ni Kiba mwenyewe aliyeamua kumuacha yeye na kuoa mtu mwingine, na wala si yeyote yule ambaye yupo karibu na Kiba,”
Amesema mbali na hilo, pia anahisi hivyo maana tofauti na zamani Jokate alipokuwa akitazama vitu vyake mitandaoni na kumsapoti lakini siku hizi mrembo huyo hafanyi.
Buheti amesema kuwa kama ni kweli Jokate atakuwa ananichukia kisa mpenzi wake wa zamani Kiba kuoa kama watu wanavyosema, basi atakuwa ananichukia bure.