Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka na kusema kuwa licha ya umaarufu mkubwa alionao lakini ataendelea kuishi maisha ya kawaida ya kutojionyesha katika jamii.
Alikiba amesema kuwa maisha anayoishi ndio anaona yanafaa zaidi machoni kwa mashabiki wake ambao walimpokea kipindi hana kitu kabisa.
Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa hawezi kubadili maisha yake halisi aliyokuwa anaishi kabla ya kuunza muziki miaka ya 20000 mpaka kujulikana.
Kiba amesema kuwa watanzania walimpokea katika hali ambayo kiukweli haisemeki sasa hii leo ni vigumu sana kubadilika na kuishi maisha ya ustaa sana.
Ameongeza kwa kusema kuwa yeye ni staa atafanya na ataishi maisha ambayo amechagua lakini bado ataendea kuwa karibu na watu wake.
Mwanamuziki huyo kwasasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Mvumo wa Radi ambao unafanya vizuri.