Mwanamitindo Hamisa Mobetto amefunguka kuhusu taarifa zilizodai kuwa amepigwa na mama mzazi wa Diamond Platnumz, Sanura Kassim ‘Sandra’.

Hamisa alipata time ya kuzungumza na waandishi wa habari na kusema jambo hilo ni binafsi zaidi ila kugombana kwa binadamu ni kitu cha kawaida.

“Hilo siwezi kuliongelea, yeah!. is too person, is too private, is too family. Hata vikombe kwenye kabati vinagong’ana, so sisi binadamu vinaweza kutokea,”.

Alipoulizwa iwapo kwa sasa yeye na mama Diamond wana maelewano mazuri, alijibu; ‘Sina kinyongo na mtu, sina bifu na mtu, mimi am just fine, may be yeye mwenyewe sio upande wangu wa kuweza kuelezea,’.

Taarifa za Hamisa kupigwa na mama Diamond zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii siku Jumatatu ya wiki iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *