Mwanamitindo Nikki Bella na mkali wa mchezo wa mieleka, John Cena, wamemaliza tofauti zao na kurudiana baada ya kudaiwa kuachana.

Wawili hao ambao walitangaza kuwa wapo kwenye mipango ya kufunga ndoa, walidaiwa kuachana mapema mwezi uliopita, lakini mwishoni mwa wiki iliyopita walionekana wakiwa pamoja kwa mara ya kwanza.

Mastaa hao walionekana wakiwa wanaelekea kunywa kahawa kwenye Mji wa San Diego huko California. Hata hivyo, Cena alifunguka na kusema kila kitu kipo sawa.

Amesema kuwa “Bado ninampenda Nikki, bado nina lengo la kutaka kufunga ndoa na Nikki, bado ninatarajia kuwa na familia na Nikki,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *