Muigizaji wa Bongo movie Blandina Chagula ‘Johari’ amesema kuwa yupo tayari kwa aliyekuwa mpenzi wake, Ray kufunga ndoa na mzazi mwenzake Chuchu Hans.
Johari amesema kuwa kwa upande hajisiki vibaya kama wawili hao wakioana kwasababu yeye alishaachana na Ray hivyo hakuna sababu ya kuona wivu wawili hao wakiona.
Johari na Ray walikuwa kwenye Mahusiano ya kimapenzi kwa miaka mingi kipindi cha nyuma lakini ameibuka na kuweka wazi kwa hivi sasa hana kinyongo na wapendanao hao kuwa pamoja.
Johari amedai kuwa hakuna kitu kitakachomfurahisha kama mwigizaji mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’ akimuoa mzazi mwenziye, Chuchu Hansy.
Pia Johari ameweka wazi kuwa Chuchu ni chaguo sahihi la Ray maana ni mwanamke ambaye amemzalia mtoto mzuri.