Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy ameingiza sokoni bidhaa zake za Sabuni na mafuta akishirikiana na kampuni ya Grace Products Ltd.

Nandy amekuwa miongoni mwa mastaa wachache ambao wameamua kujikita katika biashara ndogondogo ukiachilia mbali na biashara ya muziki inayokidhi maisha yao ya kila siku.

Miongoni mwa mastaa wanaomiliki brands za bidhaa zao ni pamoja na muigizaji Aunty Ezekiel ambaye anamiliki Body Spray zake.

Wengine ni Shilole ambaye nae ametoa Chilli sauce za brand yake na Rosa Ree ambaye anamiliki Rosa Ree Mini Super Market.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *