Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi wa mamlaka hiyo, Richard Kayombo amesema ulipaji wa aina hiyo ya kodi umekuwa na changamoto kubwa ya kutolipwa kwa wakati, ambapo wamiliki wa nyumba hawalipi kodi kabisa na wengine hudanganya viwango halisi vya kodi ya kupangisha.
Kayombo amefafanua kwamba, kiasi cha kodi kunachotakiwa kulipwa kwa serikali ni asilimia kumi ya gharama ya pango na kuwataka wamiliki kuweka wazi gharama halali za kodi wanazowatoza wapangaji na wale ambao watabainika kudanganya watachukuliwa hatua za kisheria.
Vile vile amesema watu waache kupotoshana kuhusu mpango huo kwakuwa ni mahususi kwa serikali katika kuhakikisha wanasimamia vyanzo vyake vya mapato ili kufikia nchi yenye kipato cha kati na kufikia malengo ya milenia waliyojiwekea.